Diego Costa kuikosa Ufaransa leo

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo Chelsea, alipatiwa matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata wakati akiwa kwenye mazoezi na timu hiyo ya taifa.

Hispania. Uongozi wa timu ya Taifa ya Hispania umeieleza timu ya Chelsea kwamba mshambuliaji wake, Diego Costa amelazimika kuondolewa kwenye timu ya Taifa kutokana na kuumia enka wakati wa mazoezi ya timu hiyo.

Mshambuliaji huyo Chelsea, alipatiwa matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata wakati akiwa kwenye mazoezi na timu hiyo ya taifa.

Costa alilazimika kutolewa na kocha Julen Lopetegui baada ya kuumia lakini majibu ya X-Rays yalionyesha  hakukuwa na majeraha makubwa.

Vinara hao wa Ligi Kuu England walitaarifa kwamba mshambuliaji huyo ataendelea kuwa chini ya uwangalizi wa  wa madaktari wa timu ya taifa ya Hisapania kutokana na kikosi hicho kuwa na mechi ya kirafiki leo dhidi ya Ufaransa.