Gundogan amkubali Gabriel Jesus

Muktasari:

  •  Jesus alitua rasmi Man City kwenye dirisha la Januari na tangu atue kwenye kikosi hicho kwa muda mfupi ameonyesha makali yake kabla ya kuumia na kukosa mechi kadhaa za mwishoni mwa msimu.

Kiungo, Ilkay Gundogan amesema Manchester City imefanya kitu cha msingi kweli kwa kumsajili mshambuliaji wa Gabriel Jesus kwenye kikosi chao msimu uliopita.

 Jesus alitua rasmi Man City kwenye dirisha la Januari na tangu atue kwenye kikosi hicho kwa muda mfupi ameonyesha makali yake kabla ya kuumia na kukosa mechi kadhaa za mwishoni mwa msimu.

Staa huyo alifunga mabao saba katika mechi nane za Ligi Kuu England kabla ya kukaa nje kwa kipindi kirefu kutokana na kuwa majeruhi.