Sunday, March 19, 2017

Lwandamina: Mapambano ndio yameanzakocha wa Yanga, George Lwandamina

kocha wa Yanga, George Lwandamina 

By Gift Macha, Lusaka

Baada ya Yanga kutupwa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, kocha wa timu hiyo, George Lwandamina ameijipanga kuwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Zanaco ya mjini hapa kwa faida ya bao la ugenini kutokana na matokeo ya jumla ya bao 1-1 Dar es Salaam na Lusaka timu hizo zikatoka suluhu.

Lwandamina, ambaye aliiongoza Zesco United ya Zambia kufika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka jana, amesema kwa namna timu yake ilivyocheza dhidi ya Zanaco, wana nafasi kubwa ya kufika mbali.

"Kupelekwa tu katika kombe la Shirikisho ni nafasi tosha kwetu, hatuwezi kulala na kuacha kuitumia. Ukitazama namna timu yetu ilivyocheza ni dhahiri kwamba tuna uwezo wa kufika mbali," alisema Lwandamina.

-->