Makocha Serengeti Boys wachimba mkwara Congo

Muktasari:

Makocha hao aliyasema hayo wakati anaendelea kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi ya Congo utakaofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Alphonse Massamba-Debat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville.

Congo. Makocha wa timu ya Taifa ya vijana wa Tanzania ‘Serengeti Boys’, Bakari  Shime na Muharami Mohammed wamesema wapo tayari kwa vita.
Makocha hao aliyasema hayo wakati anaendelea kufanya maandalizi ya mwisho ya mchezo dhidi ya Congo utakaofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Alphonse Massamba-Debat ulioko kwenye Makutano ya Barabara za Nkolo na Boko, hapa jijini Brazzaville.
Shime anasema: “Timu iko vizuri. Tumejiandaa vizuri kwa yale ya msingi yote tumekamilisha. Kwa hivyo, kila kitu kiko sawa, kama tulivyokusudia. Tupo hapa Congo kwa sasa kumalizia au kukumbushia mambo mawili au matatu hivi.
 “Tupo hapa Congo kuzoea hali ya hewa. Kwa bahati nzuri si tofuati na ya nyumbani Tanzania,” anasema Shime kwa kujiamini kabisa leo mchana Septemba 29, 2016 huku akijiandaa kwenye mazoezi.
Kocha wa Makipa, Muharami au Shilton, anasema: “Silaha zangu ziko tayari kwa vita, makipa wangu wangu wote akiwamo Kelvin Kayego, Ramadhani Kabwili na Brazio wote wako fiti. Yeyote kati yao anaweza kucheza.”