Wageni kwa Simba bado!

Muktasari:

Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitisha kanuni ya wachezaji saba wa kigeni kuwamo kwenye vikosi vya klabu za Ligi Kuu msimu uliopita, kisha kuanzishia tuzo yao (wachezaji wa kigeni), ambayo msimu uliopita imetwaliwa na kiungo Thabani Kamusoko wa Yanga kwa mara ya kwanza, Simba ina safari ndefu na ngumu kuelekea kwenye kupata wachezaji bora wa kigeni

Dar es Salaam. Ikilinganishwa na Yanga na Azam zinaoonekana kuwa makini kwenye usajili wa wachezaji wa kigeni, Simba imekuwa ikifanya kwa pupa au ina kasoro kwenye utaratibu wa kusaka wachezaji hao.

Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitisha kanuni ya wachezaji saba wa kigeni kuwamo kwenye vikosi vya klabu za Ligi Kuu msimu uliopita, kisha kuanzishia tuzo yao (wachezaji wa kigeni), ambayo msimu uliopita imetwaliwa na kiungo Thabani Kamusoko wa Yanga kwa mara ya kwanza, Simba ina safari ndefu na ngumu kuelekea kwenye kupata wachezaji bora wa kigeni.

Uchambuzi wa gazeti hili kuhusu usajili wa wachezaji wa kigeni ndani ya Simba kwa miaka minne iliyopita, unaonyesha kuwa  imeuvaa mkenge kwa kusajili baadhi yao waliotimuliwa baada ya muda mfupi.