Thursday, April 20, 2017

 

Chelsea, Spurs wateka kikosi cha mwaka England


London, England. Chelsea na Tottenham Spurs kila moja inawachezaji wanne katika orodha ya kikosi bora cha mwaka cha Ligi Kuu England kilichotwaja na Professional Footballers.

Mabeki Gary Cahill, David Luiz na viungo N'Golo Kante na Eden Hazard wameiwakilisha Chelsea.

Tottenham nayo imetoa beki Kyle Walker na Danny Rose, kiungo Dele Alli na mshambuliaji Harry Kane.

Kipa wa Manchester United, David de Gea, na winga wa Liverpool, Sadio Mane na mshambuliaji  wa Everton, Romelu Lukaku wametajwa katika kikosi hicho.

Timu hiyo ya mwaka imetangwa wakati wakielekea katika sherehe za 44 za Tuzo za PFA, zitakazofanyika Jumapili ijayo jijini London.

Katika tukio hafla hiyo pia mchezaji bora wa mwaka waPFA na mchezaji chipukizi wa mwaka watatangazwa.

Kura za kuchagua wachezaji hao zinapigwa na wajumbe wa PFA ambao ni wachezaji wa klabu 100 za Ligi Kuu na ligi ndogo pamoja na Ligi ya Wanawake.

-->