Thursday, April 20, 2017

 

Real kama siyo De Gea ni Courtois


London, England
Real Madrid inataka kuvunja rekodi ya usajili wa kipa kwa kutangaza kuwa ipo tayari kutoa pauni 60milioni ili kumnasa David De Gea.

Miamba hiyo ya Hispania wamechanganyikiwa kwa De Gea na sasa wapo tayari kutoa dau mara mbili ya waliyotangaza kwanza kwa ajili ya kipa huyo.

Kama watashindwa kufikia makubaliano na kipa huyo namba moja wa Manchester United basi watageukia kwa kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois.

Chanzo kutoka Madrid kinasema kuwa: “De Gea ndiye chaguo lao la kwanza.

“Tunategemea atasaini mkataba mwisho wa msimu.”

Kama uhamisho huo utafanikiwa basi utavunja rekodi ya sasa ya usajili wa kipa kwa pauni 32.7milioni walizolipa Juventus kwa Parma kumnunua Gigi Buffon mwaka 2001.

De Gea, 26, alitakiwa kujiunga na Real Madrid mwaka 2015, lakini klabu hizo mbili zilishindwa kukubaliana dau la pauni 30 milioni katika siku ya mwisho ya usajili.

-->