Mayay-Vyombo vya habari ni mhimili katika michezo

Muktasari:

  • Akizungumzakatika hafla ya uzinduzi wa mwonekano mpya wa gazeti la Mwanaspoti, Mayay alisema ni vyema waandishi wakafahamu michezo yote ili kutoa wigo mpana wa michezo mingi kuripotiwa katika vyombo vyao.

 Aliyekuwa mgombea urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ally Mayay amesema waandishi wa habari wana mchango mkubwa katika maendeleo ya soka hapa nchini.

Akizungumzakatika hafla ya uzinduzi wa mwonekano mpya wa gazeti la Mwanaspoti, Mayay alisema ni vyema waandishi wakafahamu michezo yote ili kutoa wigo mpana wa michezo mingi kuripotiwa katika vyombo vyao.

“Vyombo vya habari vina jukumu kubwa kwa jamii mbali na kuelimisha vinatoa msukumo unaosaidia kuchukuliwa hatua za kiutendaji,”alisema Mayay, aliyegombea urais kwenye uchaguzi wa TFF uliofanyika hivi karibuni Mkoani Dodoma.

Mayay alitaja baadhi ya hatua zilizochukuliwa na TFF kufuatia msukumo wa gazeti la mwanaspoti ni kuunda programu za soka la vijana kabla ya Tanzania kushiriki fainali za Afrika za 2017 zilizofanyika nchini Gabon.