Azam yajipigia Cosmopolitan

Beki wa Azam, Shomari Kapombe (kushoto) akiwania mpira na beki wa Cosmopolitan, Ali Kabunda wakati wa mchezo wa Kombe la FA uliofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi. Azam ilishinda 3-1. Picha na Said Khamis

Muktasari:

  • Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam ilibidi kusubiri hadi dakika ya 70  kupata bao la kwanza lililofungwa na nahodha John Bocco akimalizia mpira uliookolewa vibaya na kipa wa Cosmopolitan, Geroge Kijumbe kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Dar /Musoma. Azam imeichapa Cospolitan mabao 3-1, wakati Stand United ikiibamiza Polisi Mara mabao 2-0 katika michezo ya Kombe la Shirikisho (FA) iliyofanyika jana.
Mabingwa wa Kombe la Mapinduzi, Azam ilibidi kusubiri hadi dakika ya 70  kupata bao la kwanza lililofungwa na nahodha John Bocco akimalizia mpira uliookolewa vibaya na kipa wa Cosmopolitan, Geroge Kijumbe kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha Azam ambayo katika dakika 76 ilipata bao la pili lililofungwa na Shaban Iddi kabla ya Joseph Mahundi kufunga bao la tatu dakika ya 79, huku Cosmopolitan ikipata bao la kufutia machozi dakika ya 78 lililofungwa na Fidelis Kyangi.
Katika mchezo mwingine wa mashindano hayo, Frank Khamis alifunga mabao mawili wakati yake ya Stand United ilipoichapa Polisi Mara 2-0 kwenye Uwanja wa Karume, Musoma.