Azam yalia ubovu wa Nangwanda Sijaona

Muktasari:

  • Azam ililala kwa mabao 2-1 kutoka kwa Ndanda Jumamosi iliyopita ikiwa ni mechi yake ya pili kupotea msimu huu.

Dar es salaam. Klabu ya Azam imesema kipigo cha mabao 2-1 ilichokipata kutoka kwa Ndanda kimechangiwa na ubovu wa sehemu ya kuchezea kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Azam ililala kwa mabao 2-1 kutoka kwa Ndanda Jumamosi iliyopita ikiwa ni mechi yake ya pili kupotea msimu huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana baada ya kurejea kutoka Mtwara, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Azam, Jafar Idd alisema licha ya kukubali kipigo hicho, uwanja umechangia matokeo hayo mabaya kwao.

“Tunakubali matokeo, lakini Uwanja wa Nangwanda si mzuri, hasa sehemu ya kuchezea. Hata Ndanda nao uliwasumbua,” alisema Idd.

Katika hatua nyingine; Idd amesema beki mahiri wa timu hiyo, Pascal Wawa aliyekuwa nje kwa muda mrefu atarejea katika mchezo ujao dhidi ya Ruvu Shooting.