Balotelli ni bure kaibisaa! Nice yatunguliwa mabao 2-0

Italia. Washambuliaji wa Nice, Mario Balotelli na Wesley Sneijder wameshuhudia klabu yao  ikizamishwa mabao 2-0 dhidi ya Napoli katika mechi ya makundi kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya jana Jumanne na kufanya matokeo ya jumla kuwa 4-0.

Mshambuliaji Balotelli analaumiwa na kocha wake kutokana na kushindwa kuisaidia timu hiyo ambayo matumaini yao makubwa ilikuwA kushinda mchezo huo.

Balotelli alikosa mechi ya kwanza kutokana na kuwa majeruhi lakini kurejea kwake uwanjani hakukuwa na athari yoyote kwa wapinzani wao jambo lililowapa nafasi washambuliaji wa Napoli kufika langoni mara kwa mara.