Bayern Munich wapania mataji kumfunika Guardiola

Ujerumani. Beki wa Bayern Munich, Rafinha amesema anaamini kwamba timu yake ipo kwenye kiwango kizuri cha kunyakua mataji katika msimu huu ukilinganisha kipindi ambacho timu hiyo ilikuwa chini ya Pep Guadiola.

Bayern Munich  imejiimarisha kileleni kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Bundesliga na inakabiliwa na mchezo wa robo fainali na nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi huu.

Timu hiyo iliwahi kuwa chini ya Guardiola aliyeifanikisha kutwaa mataji, lakini baadaye alijiunga na Barcelona akichukua mikoba ya Jupp Heynckesmsimu wa 2012-12.

Swali la kujiuliza kwenye klabu hiyo kutokuwapo Guardiola pamoja na kuwapo majeruhi itakuwa kikwazo kwa miamba hao kushindwa kutwaa mataji msimu huu?