Benchi lamfanya kipa wa Simba kutaka kuvunja mkataba kusaka nafasi ya kucheza sehemu nyingine

Muktasari:

  • Kissu alikuwa kipa namba nne katika kikosi cha Simba hivyo kuamua kutafuta timu nyingine ambayo itampa nafasi ya kucheza.

Kipa wa Simba, David Kissu aliyekuwa akicheza kwa mkopo Toto Africans  ameamua kuvunja mkataba na timu hiyo ya Msimbazi ili aweze kuanza maisha mapya kwingine.

Kissu alikuwa kipa namba nne katika kikosi cha Simba hivyo kuamua kutafuta timu nyingine ambayo itampa nafasi ya kucheza.

Kipa huyo amefungua milango kwa Toto Africans alipokuwa chaguo la kwanza hadi iliposhuka daraja msimu uliopita.

Kissu alisema ameamua kuachana na mabingwa hao wa Kombe la FA kutokana na ufinyu wa nafasi ya kucheza na sasa yupo katika mazungumzo na baadhi ya timu za Ligi Kuu.