Blagnon, Kichuya waipandisha ndege Simba

Muktasari:

Uamuzi ulisababisha wachezaji wa Mbao kumvaa mwamuzi Kikumbo wakipinga uamuzi huo na kusababisha askari kuingia uwanjani kutuliza ghasia.

Dodoma. Simba imetwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho Azam kwa kuifunga Mbao kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na kufuzu kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.

Simba ilipata mabao yake mawili yaliyofungwa na washambuliaji wake Fredrick  Blagnon na penalti ya Shiza Kichuya wakati bao la kufutia machozi kwa Mbao lilifungwa na Ndaki Robert.

Katika mchezo huo wa fainali timu zote mbili zilicheza kwa nguvu na kujilinda kwa umakini hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika timu hizo zilikuwa suruhu.

Kipindi cha pili kila timu ilifanya mabadiliko lakini uamuzi wa Joseph Omog kumtoa Said Ndemla dakika 83 na kuingia Fredrick Blagnon uliokuwa ni habari njema kwa Simba.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alifungia Simba bao la kwanza katika dakika 95, lakini Mbao ilisawazisha dakika 109 kupitia Ndaki.

Wakati mashabiki wakiamini mechi hiyo itakwenda kwenye penalti katika dakika 116, uamuzi wa utata wa mwamuzi Mohamed Kikumbo ulifaidisha Simba kwa kupata penalti.

Uamuzi ulisababisha wachezaji wa Mbao kumvaa mwamuzi Kikumbo wakipinga uamuzi huo na kusababisha askari kuingia uwanjani kutuliza ghasia.

Baada ya vurugu hizo mpira uliendelea kwa Kichuya kupiga penalti hiyo na kuifungia Simba bao la pili na ushindi na kuamsha shangwe uwanjani hapo.

Awali milango ya Uwanja wa Jamhuri ulifungwa saa 8.00 mchana baada ya majukwaa yote kujaa. Ukikadiriwa kutimiza idadi ya mashabiki 23,000  idadi iliyotangazwa na shirikisho la soka Tanzania (TFF)  na chama cha soka Dodoma (Dorefa)

Kitendo cha timu ya Simba kutoonekana wakishuka kwenye basi uwanjani  kimeonekana kuwashangaza mashabiki wengi waliofika kutazama pambano hili la fainali.

Mchezo huo unaochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma umevuta hisia nyingi za mashabiki waliofurika na kujaza uwanja huu.

Lakini katika hali isiyotarajiwa na wengi basi la timu ya Simba SC lililoingia uwanjani lilikua tupu na waliokua ndani yake ni wachezaji wanne pekee.

Baada ya basi hilo kuingia ndani baadhi ya mashabiki walibaki kujiuliza walipo wachezaji hao.

Wachezaji wa Simba kabla ya kuanza mpira wote waliinama na kufunga viatu vyao wakati wa Mbao walienda kupiga magoti kwenye lango lao

Simba ilianzisha mpira kwa kuupiga nje jambo ambao ni kushangaza katika soka.

Simba ilianza mechi kwa kasi na dakika ya 10, Laudit Mavugo anapiga shuti linalopaa akishindwa kumalizia mpira uliookolewa vibaya na mabeki wa Mbao

Mbao ilijibu mapigo kupitia Pius Buswita nusura aipatie bao akishindwa kumalizia mpira uliotemwa na kipa Daniel Agyei wa Simba kutokana na faulo ambayo ilipigwa na Jamal Mwambeleko

Dakika ya 34, Mavugo anapiga shuti linalombabatiza Yussuf Ndikumana na kuwa kona ambayo haijazaa matunda.

Jamal Mwambeleko wa Mbao anapewa kadi ya njano dakika ya 43 kwa kumchezea rafu Mohammed Hussein 'Tshabalala'

Kabla ya kipindi cha pili kuanza, mmoja wa wachezaji wa Mbao alienda kumwagia maji milingoti ya lango lake ikiashiria kama imani za kishirikina.

Dakika ya 54 mshambuliaji wa Mbao, Habib Hajji anakosa bao la wazi kwa kupiga nje.

Mbao wanafanya mabadiliko anatolewa George Sangija na kuingia Dickson Ambundo wakati

Simba inamtoa Juma Luizio na kuingia Ibrahimu Ajib

Dakika ya 51, Simba wanamtoa Mohammed Hussein na kumuingiza Abdi Banda, dakika 83, Simba inamtoa Ndemla anaingia Blagnon.