Bondia Francic Cheka ataja sababu za kuchezea kipigo Uswisi

Muktasari:

  • Cheka alipigwa kwa pointi za majaji 3-0 kwenye pambano hilo la raundi nane la uzani mwepesi wa juu (kg 81) lililofanyika mjini Geneva.

Usiku wa kuamkia leo Jumapili, bondia Francis Cheka alichezea mkong'oto kwenye pambano na Enes Zecirevic huko Uswisi.

Cheka alipigwa kwa pointi za majaji 3-0 kwenye pambano hilo la raundi nane la uzani mwepesi wa juu (kg 81) lililofanyika mjini Geneva.

"Nisingeweza kushinda kwa pointi, nilijua matokeo yale baada ya kumaliza raundi zote. Siku zote unapocheza ugenini na kumaliza raundi zote ni vigumu kupewa ushindi dhidi ya mwenyeji, ndivyo ilivyokuwa hata na kwangu.

"Nimeumizwa kuharibu rekodi yangu, lakini sijashangazwa na kupigwa kwa pointi kwani ni ushindi ambao yoyote anaweza kupewa," alisema Cheka