Bondia Joshua kumvaa Pulev Okt 28

Muktasari:

Joshua atarejea ulingoni kwa mara ya kwanza tangu alipopata ushindi wa kishindo dhidi ya Wladimir Klitschko kwenye Uwanja wa Wembley mwezi Aprili na sasa atamvaa Pulev kwenye Uwana wa Principality hapo Oktoba. 28.

Bingwa wa dunia ngumi uzito wa juu Anthony Joshua atatete ubingwa wake dhidi ya bondia wa Bulgaria, Kubrat Pulev.

Joshua atarejea ulingoni kwa mara ya kwanza tangu alipopata ushindi wa kishindo dhidi ya Wladimir Klitschko kwenye Uwanja wa Wembley mwezi Aprili na sasa atamvaa Pulev kwenye Uwana wa Principality hapo Oktoba. 28.

"Oktoba 28 naona kama ni mbali, nilikuwa natamani kurudi ulingoni tangu siku ile niliposhinda Wembley, lakini sasa siku imethibishwa tayari," alisema Joshua bingwa wa WBA na IBF.

"Nitajifungia ndani kujiandaa na pambano langu la 20 litakalofanyika wiki nane zijazo. Navutiwa na mazingira ya uwanja wa Principality lengo langu ni kuwapa mashabiki burudani ya kutosha usiku huo."

Pulev atakuwa akipigana pambano lake la pili la kuwania ubingwa wa dunia baada ya kupigwa na Klitschko mwaka 2014 na alisema yuko tayari kumvaa Mwiingereza huyo mbele ya mashabiki 80,000.

"Anthony ni bondia mzuri na mpinzani bora, lakini aina yake ya upiganaji inafanana na yangu," Pulev aliandika katika ukurasa wake wa Facebook.