Canavaro: Tutapigana hadi tone la mwisho

Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ .

Muktasari:

  • Yanga inaburuta mkia katika Kundi A kwa kuwa na pointi moja waliyoipata kwenye michezo mitatu, huku TP Mazembe ya DR Congo ikiongoza kwa kujikusanyia pointi saba hadi sasa.

Takoradi, Ghana. Nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amesema kikosi chao hakijapoteza morali licha ya kuwa wa mwisho katika kundi lao na mchezo wa leo una umuhimu mkubwa.

Yanga inaburuta mkia katika Kundi A kwa kuwa na pointi moja waliyoipata kwenye michezo mitatu, huku TP Mazembe ya DR Congo ikiongoza kwa kujikusanyia pointi saba hadi sasa.

Akizungumza baada ya mazoezi jana asubuhi mjini Takoradi, Cannavaro alisema anajua ni kiwango watakachokutana na ugumu katika mchezo wao wa leo, lakini wapo imara kukabiliana na hali yeyote.

“Yanga imeshacheza mechi nyingi za ugenini na mazingira mara nyingi yanakuwa na changamoto kubwa, lakini bado hilo siyo tatizo kwetu.Tulishacheza katika mazingira magumu mno nchini Angola na tukafuzu kwa hatua hii, nadhani ni kujipanga na kuangalia tunataka nini kwa ajili ya kusonga mbele,” alisema nyota huyo.