Cech kuinyoosha Chelsea fainali FA

Muktasari:

Cech alishinda mataji ya Ligi Kuu na Kombe la FA mara nne wakati akiwa na Chelsea, pia Kombe la Ligi na Ligi ya Mabingwa pamoja na Ligi ya Europa  kabla ya kujiunga na Arsenal mwaka 2015.

London, England. Kipa wa Arsenal, Petr Cech amefurahia kukutana na klabu yake ya zamani ya Chelsea kwenye fainalia ya Kombe la FA.

Cech alishinda mataji ya Ligi Kuu na Kombe la FA mara nne wakati akiwa na Chelsea, pia Kombe la Ligi na Ligi ya Mabingwa pamoja na Ligi ya Europa  kabla ya kujiunga na Arsenal mwaka 2015.

Chelsea hivi sasa wanalisogelea taji la ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara nyingine na wanatarajia kucheza mechi yao ya fainali Mei kwenye Uwanja wa Wembley baada ya kuisambaratisha Tottenham mabao 4-2 katika  fainali iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hata hivyo, Arsenal ilikiwa na kibarua kingine Jumapili wiki hii kwenye mchezo wa Ligi Kuu ilipomenyana na Manchester City na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 ikiwa ni mechi yao ya kumbukumbu.

Alisema, “Ndio itakuwa mechi ya kipekee. Kila tunapokutana kwenye Kombe la FA  unakuwa mechezo wenye ushindani. Nitacheza dhidi ya timu yangu iliyonipa mafanikio makubwa kwa miaka iliyopita.”