Monday, March 20, 2017

Conte ajisifu kikosi chake cha Chelsea

 

London, England. Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amesema kwamba anatarajia kikosi chake  kitaimarika zaidi na kuendana na mbinu na mawazo yake wanapoelekea ukingoni kwenye Ligi Kuu ya England.

Timu hiyo inayoongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, mwishoni mwa wiki hii ilijiimarisha kileleni baada ya kuifunga Stock City kwa mabao 2-1 na kufanya kuwapo na tofauti ya pointi 13 dhidi ya timu inayoifuatia Tottenham.

Chelsea imefuzu nusu fainali ya Kombe la FA. Raia huyo wa Italia, anaamini wamba timu yake imeanza kushika falsafa yake na alisisitiza kwamba kikosi chake kitaimarika zaidi kutokana na kutumia muda wake mwingi kwenye mazoezi klabuni hapo.

-->