Conte amfangilia Wenger

London, England. Kocha wa Chelsea, Antonio Conte amesema Arsene Wenger ataendelea kuwa moja wa makocha bora duniani hata kama Arsenal watakosa ubingwa wa Kombe la FA.

Wenger (67), amekuwa kocha wa Gunners tangu1996 na mkataba wake wa sasa unaelekea mwishoni.

Wenger amekutana na maandamo mfululizo msimu huu kutoka kwa mashabiki wake wa Arsenal wakimtaka ajiuzuru wadhifa wake.

Lakini mwisho wa msimu huu anaweza kuondoka na taji lake la saba la Kombe la FA wakati akikaribia rekodi ya Liverpool.

Conte anaamini Wenger ataendelea kuwa kocha wa Arsenal msimu ujao.

Wenger alisema hatma yake itamuliwa na kikao cha bodi kitakachokutana leo baada ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Blues.

"Najua vizuri kuwa Arsene Wenger amefanya kazi nzuri katika Kombe la FA na kutwaa mataji mengi," alisema Conte.