Conte atisha mkutano wa dharura mazoezi kujiokoa kutimuliwa Chelsea

Muktasari:

  • Chelsea ilianza vibaya mchezo wake wa kwanza, baada ya kufungwa na Burney mabao 3-2 kwenye mchezo wake wa Jumamosi wiki iliyopita jambo lililomweka roho juu kocha huyo.

London, England. Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ameitisha mkutano wa dharura cha wachezaji wake ili kuwaongezea morari kwenye mchezo wa Ligi Kuu England unaofuata dhidi ya Tottenham ili kuepuka kutimuliwa mapema kikosini hapo.

Chelsea ilianza vibaya mchezo wake wa kwanza, baada ya kufungwa na Burney mabao 3-2 kwenye mchezo wake wa Jumamosi wiki iliyopita jambo lililomweka roho juu kocha huyo.

Hii si mara ya kwanza kuitisha mkutano tangu kikosi hicho kipoteze mchezo wake wa kwanza, taarifa zinaeleza kwamba amekuwa akiitisha mikutano ya mara kwa mara ili kuwajenga kisaikolojia wachezaji wake.