Costacurta: Neymar ni zaidi ya Ronaldo, Messi

Muktasari:

Nyota huyo wa zamani wa AC Milan na Italia amedai kuwa Mbrazili huyo amefikia katika viwango sawa na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.


Bingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa, Alessandro Costacurta amesema Neymar kwa sasa ni mchezaji bora wa dunia.

Nyota huyo wa zamani wa AC Milan na Italia amedai kuwa Mbrazili huyo amefikia katika viwango sawa na Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Costacurta aliimbia Sky Italia: “Naamini kwa wakati huu Neymar ni bora zaidi ya Cristiano Ronaldo na Messi, yeye ni mchezaji bora wa dunia kwa sasa mwaka huu 2017.

“Kama utaangalia uchezaji wao wa sasa na kuwalinganisha  Messi na Ronaldo, nafikiri Neymar ni bora kwa sasa.”

Beki huyo aliongeza kuwa katika maisha ya nje Neymar anafanana zaidi na Ronaldo kuliko Messi.

Costacurta alisema: “Maisha binafsi ya Neymar yanafafana sana na Ronaldo. Amekuwa bize kwenye mitandao ya kijamii, lakini bado hajafikia viwango vya Ronaldo.”