Dakika 6 zamnyima Simbu Sh200 mil>

Muktasari:

Simbu alimaliza katika nafasi ya tano akikimbia kwa saa 2:09:10 alishindwa kuweka rekodi ya ubingwa na kuondoka na kitita cha dola 100,000 (milioni 200 za Tanzania), ambazo ziliwekwa kama motisha kwa mkimbiaji ambaye angetumia saa 2:03 au chini ya muda huo kumaliza mbio hizo zilizoanzia kwenye viwanja vya Green Park jana asubuhi

 Dakika sita zinaweza kuonekana ndogo, lakini jana zimemkosesha kitita cha Sh 200 milioni mwanariadha, Alphonce Simbu katika mbio za London Marathoni.Simbu alimaliza katika nafasi ya tano akikimbia kwa saa 2:09:10 alishindwa kuweka rekodi ya ubingwa na kuondoka na kitita cha dola 100,000 (milioni 200 za Tanzania), ambazo ziliwekwa kama motisha kwa mkimbiaji ambaye angetumia saa 2:03 au chini ya muda huo kumaliza mbio hizo zilizoanzia kwenye viwanja vya Green Park jana asubuhi. (Imani Makongoro