Friday, August 11, 2017

Dauda: Nipo tayari kwa lolote

 

By MWANAHIBA RICHARD

Mgombea wa nafasi ya ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi mkuu wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Shafii Dauda amesema  ametumia demokrasia kugombea nafasi hiyo yupo tayari kwa matokeo yoyote.

Awali Dauda alitangaza kujitoa kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kuwepo na tuhuma zilizomuhisisha kwamba alihisiwa na vitendo vya rushwa jijini Mwanza ambapo alihojiwa na Takukuru na kuachiwa.

Dauda alitangaza kujitoa kugombea nafasi hiyo kwa madai kwamba uchaguzi huo unaonekana kujaa siasa za kuharibiana na kuchafuliana majina, lakini watu wake wa Karibu walimshauri kukata rufaa ili kupigania haki yake.

"Ni kweli nilijitoa ila washauri wangu baadaye walinishauri kukata rufaa na ndiyo maana nimerejea baada ya kubainika kwamba hazikuwa na ukweli wowote tuhuma hizo, natumia demokrasia ambayo ni haki ya kila mtu lakini kuchaguliwa ama kutochaguliwa inabaki kwa wapiga kura.

"Unapitumia demokrasia basi siyo lazima uchaguliwe ndivyo ilivyo hata kwangu nisipochaguliwa maisha mengine yanaendelea na mambo yangu ambayo nayafanya yatafanyika kama kawaida," alisema Dauda.

Dauda alisema anaendelea na kampeni zake za kunadi sera pamoja na kuomba kuchaguliwa kama wapiga kura hao 130 watakubali aingie madarakani kuwawakilisha.

-->