Defoe aibeba England

Muktasari:

Mshambuliaji huyo wa Sunderland mwenye miaka 34, alichezea kwa mara ya kwanza England tangu alipofanya hivyo Novemba 2013 na amerejea kwa kishindo kwa kufunga bao la kuongoza katika dakika 21.


Mshambuliaji Jermain Defoe amerejea katika kikosi cha England ni "habari njema" kwa mujibu wa kocha Gareth Southgate baada ya mshambuliaji huyo kufunga bao katika ushindi 2-0 dhidi ya Lithuania ukiwa ni mchezo wa kusaka kufuzu kwa Kombe la Dunia2018.

Mshambuliaji huyo wa Sunderland mwenye miaka 34, alichezea kwa mara ya kwanza England tangu alipofanya hivyo Novemba 2013 na amerejea kwa kishindo kwa kufunga bao la kuongoza katika dakika 21.

"Nimefurahi kuona Defoe amefunga bao katika mechi hii," alisema Southgate.

"Amekuwa na mchango mkubwa kwetu katika mchezo huu na mashindano kwa jumla."

England ilitegeneza nafasi chake baada ya bao la Defoe, lakini ilifanikiwa kuipenya ngome ya wapinzani wao tena katika dakika 66 wakati Jamie Vardy aliyeingia akitokea alipofunga bao la pili katika mpira wake wa kwanza kuugusa.

Southgate aliongeza: "Nimefurahi kwa wawili hawa kufunga mabao katika mchezo huu, ni habari njema kwa Jermain na mwenzake Jamie ameongeza kitu kwetu."

Huku nyota  Tottenham, Harry Kane akiwa tegemeo la timu hiyo kama itafuzu kwa Kombe la Dunia 2018,  Southgate atakuwa akitafuta washambuliaji wengine wa kumsaidia.

Jamie Vardy, Daniel Sturridge, Wayne Rooney, Andy Carroll  na Marcus Rashford watakuwa mstali wa mbele kwenye orodha yake pamoja na mkongwe Defoe, ambaye wakati wa fainali za Russia zinaanza atakuwa na miaka 35.