Demba Ba kurejea uwanjani

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Newcastle, Demba Ba

Muktasari:

  • Ba aliumia vibaya baada ya kuchezewa vibaya na nahodha wa klabu ya Shanghai SIPG, Sun Xiang akiichezea klabu yake, Shanghai Shenhua

China. Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Newcastle, Demba Ba ameanza mazoezi mepesi baada ya kufanyiwa upasuaji na daktari bingwa kutoka Ufaransa, Olivier Blinger ili kurekebisha mguu wake uliovunjika siku chache zilizopita kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya China, CSL.

Ba aliumia vibaya baada ya kuchezewa vibaya na nahodha wa klabu ya Shanghai SIPG, Sun Xiang akiichezea klabu yake, Shanghai Shenhua 

Nyota huyo wa kimataifa wa Senegal alihofiwa na wengi kuwa huo ungekuwa mwisho wake wa kucheza soka, lakini baada ya upasuaji wenye mafanikio alieleza kuwa ataweza kupona na kurudi uwanjani.

Sun Xiang ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa China aliomba msamaha akieleza kuwa haikuwa dhamira yake kumuumiza Ba.

Licha ya tukio hilo, Shenhua ilimfariji Ba kwa ushindi wa mabao 2-1 kwa bao la ushindi la Fredy Guarin.