Dharau zimeiponza Yanga

Muktasari:

  • Simba iliwatandika Yanga mabao 2-1, mabao yao yakifungwa na Laudit Mavungo na Shiza Kichuya, huku la Yanga likifungwa na Simon Msuva kwa mkwaju wa penalti.

Mwanza. Nyota wa zamani wa Express ya Uganda na Kagera Sugar, Samuel Kahabuka amesema Yanga waliwadharau Simba baada ya kupata bao na ndiyo sababu ya kufungwa.

Simba iliwatandika Yanga mabao 2-1, mabao yao yakifungwa na Laudit Mavungo na Shiza Kichuya, huku la Yanga likifungwa na Simon Msuva kwa mkwaju wa penalti.

Kahabuka alisema Yanga walikuwa na nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo, lakini waliwadharau wapinzani wao baada ya kupata bao la kuongoza.