Diamond aomboleza msiba wa mama Zari

Muktasari:

Halima (58) alikutwa na mauti jana asubuhi katika Hospitali ya Nakasero alikokuwa akitibiwa kwa takribani mwezi mmoja.

Dar es Salaam. Mwanamuziki Diamond amemfariji mkewe Zarina Hassan ‘Zari’ baada ya kuondokewa na mama yake, Halima Hasssan aliyefariki dunia jana Alhamisi asubuhi.

Halima (58) alikutwa na mauti jana asubuhi katika Hospitali ya Nakasero alikokuwa akitibiwa kwa takribani mwezi mmoja.

Nassib Abdul maarufu ‘Diamond Platnumz’ ni mume wa Zari aliyezaa naye watoto wawili; Tiffa na Nillan pia aliungana na familia hiyo katika kuomboleza msiba huo wa mkwe wake, huku akiandika kwenye ukurasa wake wa Istagram; “Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi amen”.