Dodoma nini, mambo Dar bwana!

Wachezaji wa Mtibwa Sugar.

Muktasari:

  • Timu hizo tatu zimepiga kambi zao kwa wiki kadhaa zikijiandaa kwa Ligi Kuu itakayoanza Agosti 20; Ndanda itaanza msimu mpya na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Siku zote Dar es Salaam ndiyo kila kitu. Ni jiji la maraha. Hivi ndivyo  ilivyodhihirika kwa timu za Mwadui, Ndanda na Mtibwa Sugar zilipokimbia mikoa yao na kuweka kambi zao kwa maandalizi ya msimu ujao.

Timu hizo tatu zimepiga kambi zao kwa wiki kadhaa zikijiandaa kwa Ligi Kuu itakayoanza Agosti 20; Ndanda itaanza msimu mpya na Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mtibwa Sugar itawakaribisha maafande waliopanda daraja, Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro wakati Mwadui itakuwa ugenini kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kucheza na Toto Africans.

Mwadui ndiyo ilianza kulivamia Jiji la Dar es Salaam na kuweka kambi na baadaye Mtibwa ikafuata na mwishoni mwa wiki Ndanda imetua nayo pia kuweka kambi ya muda.