England yasonga, Guinea nje

Korea Kusini. Argentina imeichakaza Guinea kwa mabao 5-0  na kuiondoa katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa vijana chini ya miaka 20 yanayoendela Korea Kusini.

Guinea imemaliza ikiwa ya mwisho katika Kundi A ilikuwa ikitaji kushinda mechi yake dhidi ya Argentina kufufua matumaini yake ya kubaki mashindano.

Mechi nyingine ya Kundi A, England imefuzu kwa hatua ya 16 bora baada ya kuwafunga wenyeji Korea Kusini kwa bao 1-0 .

Guinea imepata pointi moja katika mashindano hayo baada ya kupata 1-1 dhidi ya England, kabla ya 3-0 na wenyeji Korea Kusini.