Fabregas atangaza kuondoka Chelsea

Fabregas atangaza kuondoka Chelsea

London, England. Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas amesema ataondoka klabu hapo baada ya kuanzia benchi katika mchezo wa fainali ya Kombe la FA walioyofungwa na Arsenal kwa mabao 2-1.

Kiungo huyo Mhispania amesikitishwa na kitendo cha kuanzishia benchi na hawasiwasi kuhusu hatma yake ya baadaye ndani ya kikosi cha mabingwa hao wa England.

Kiungo mwenye miaka 30, ameanza katika michezo minne kati ya sita ya mwisho iliyocheza Blues na kumsaidia kocha Antonio Conte kutwaa ubingwa.

Katika msimu mzima kiungo huyo ameanza katika michezo 15, na muda mwingi amekuwa akitumika kama mchezaji wa akiba.

Baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea  Barcelona mwaka 2014 kwa gharama ya pauni 28milioni, alikuwa moja ya wachezaji tetegemeo wa kikosi hicho.

xxxxxxxxx