Februari 21, ulikuwa usiku wa washambuliaji wa Atletico

Muktasari:

Katika ushindi wa Atletico wa mabao 4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen washambuliaji wake watatu Antoine Griezmann, Kevin Gameiro, na Fernando Torres walifunga pamoja na kiungo Saul.

Madrid, Hispania. Mvua ya mabao ilishudiwa usiku wa Jumanne, huku asilimia kubwa ya magoli hayo yakifungwa na washambuliaji waliopita na waliopo Atletico Madrid.
Katika ushindi wa Atletico wa mabao 4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen washambuliaji wake watatu Antoine Griezmann, Kevin Gameiro, na Fernando Torres walifunga pamoja na kiungo Saul.
Katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Etihad, Sergio Aguero na Radamel Falcao walifunga mabao manne katika mchezo uliomazika kwa Manchester City kushinda 5-3 dhidi ya Monaco.
Kwa ujumla mabao saba kati ya 14 yaliyofungwa usiku wa  Februari 21 yalifungwa na washambuliaji wa Atletico, na bao la nane lilifungwa na kiungo Saul, hiyo ni ishara kwamba klabu hiyo ya jiji la Madrid ina jicho zuri la kutazama inapofika katika kutafuta mshambuliaji.