Ferguson awapa tano Man United

Muktasari:

Pia ana matumaini makubwa kwamba itafuzu mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

London, England. Kocha wa zamani wa Manchester United, Alex Ferguson amesema anaamini kwamba timu hioyo itanyakua ubingwa wa kwenye Ligi ya Europa  ikiwa ni timu pekee kutoka England.
Pia ana matumaini makubwa kwamba itafuzu mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Timu hiyo imepata matumaini ya kuwania nafasi za juu katika nne bora baada ya kupanda hadi nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Pia ina tofauti ya pointi nne dhidi ya Liverpool iliyojiimarisha nafasi ya nne yenye michezo miwili mkononi.
Manchester United ina kazi kkubwa mbeleni kutokana na kukutana na timu vigogo kwenye michezo inayofuata ambapo itakutana na Manchester City, Tottenham, Liverpool na Arsenal jambo ambalo  linaiweka timu hiyo kwenye presha ya kuwani nafasi za nne za juu kwa ajili ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.
Kocha huyo wa zamani wa Manchester United, amepata mafanikiwo makubwa alipokuwa na klabu hiyo kutokana na kunyakua mataji 38 katika miaka 27 aliyoitumikia timu hyo ya Old Trafford ikiwamo mataji mawili ya Ubingwa wa Ligi Mabingwa Ulaya jambo ambalo linaipa nguvu Manchester United kuwa na nafasi kubwa kunyakua ubingwa wa Europa. Pia wanakabiliwa na mchezo wa robo fainali utakaopigwa Aprili dhidi ya Anderlecht.
“Nina matumaini mtafanikiwa kuingia kwenye nne bora ili kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani. Nafikiri kwa hatua mliyofikia sasa ni juhudi kubwa mlizoonyesha.”
“Iwapo ikatokea mkatwaa ubingwa itakuwa itakuwa ni jambo la muhimu. Utakuwa ubingwa kwa watu wote wa Ulaya.
Haijalishi kama siyo taji la Ligi ya Mabingwa lakini bado utahesabika ni ubingwa kwa watu wa Ulaya. Pia iwapo mkishinda itakuwa mmeingia moja kwa moja kwenye Ligi ya Mabingwa. Juhudi zenu zinaonekana ni kubwa.”
“Iwapo mtashinda ubingwa wa Europa, heshima yenu itaongezeka mara dufu. Itakuwa jambo kubwa. Mkishiriki Kombe la Ulaya, Ligi ya Mabingwa Ulaya itakuwa jambo kumbwa zaidi. Tunataka pia hii iwe klabu yenye mafanikio zaidi England.”