Gabriel azichonganisha Man U na Manchester City

Gabriel Jesus

Muktasari:

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekuwa wa kwanza kueleza dhamira ya kumsajili Gabriel kutoka Palmeiras kuwa atamsajili pamoja na kinda wa Schalke 04, Leroy Sane kabla ya kufungwa kwa  dirisha la usajili mwezi ujao.

Usajili wa kinda mwenye kipaji cha kucheza soka, Gabriel Jesus raia wa Brazil unaelekea kuziingiza vitani klabu mbili za jiji la Manchester, Manchester City na Manchester United.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amekuwa wa kwanza kueleza dhamira ya kumsajili Gabriel kutoka Palmeiras kuwa atamsajili pamoja na kinda wa Schalke 04, Leroy Sane kabla ya kufungwa kwa  dirisha la usajili mwezi ujao.

Schalke  inataka Pauni 41.5 milioni kwa kinda Sane aliyeiwakilisha Ujerumani kwenye fainali za Euro 2016, ingawa imejikuta ikikwama kwa sababu ya fedha inayotakiwa kumuuza chipukizi huyo. Manchester City haitaki kulipa zaidi ya Pauni 35 milioni kwa Sane  ambaye ana miaka 18 anayetamani kucheza chini ya usimamizi wa Guardiola.

Mkurugenzi wa soka wa Schalke, Christian Heidel alikiri kukutana kwa klabu yake na City kuhusu uhamisho wa Sane.

Heidel alisema: “Kama sisi, Manchester City  inajiangalia, timu zote zinafuatilia mipango yao ya baadaye.”