Gotze kuzipa pengo la Coutinho

Muktasari:

Klopp anamtaka Gotze kuziba pengo la kiungo wake, Philippe Coutinho anayetakiwa na Barcelona.

London. Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp bado hajakata tamaa ya kuipata saini kiungo mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Mario Gotze.

Klopp anamtaka Gotze kuziba pengo la kiungo wake, Philippe Coutinho anayetakiwa na Barcelona.

Klopp alipata mafanikio na Gotze wakiwa na Dortmund miaka michache iliyopita kabla ya kiungo huyo kwenda Bayern Munich huku Klopp akitimkia Liverpool na ingawa kwa sasa Gotze ni mgonjwa, lakini Klopp amekuwa akimtaka katika kikosi chake.