Griezmann avamia anga la Messi

Muktasari:

Washambuliaji hao watatu wanaocheza katika Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ wameteuliwa kwenye tuzo hiyo ambayo imebadilishwa mfumo wake baada ya ile ya Ballon d’Or ambayo Messi na Ronaldo wamekuwa wakipokezana kwa miaka minane iliyopita.

Zurich, Uswisi. Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann ameteuliwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa mwaka 2016 akichuana na wakali Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid kwenye tuzo hizo za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Washambuliaji hao watatu wanaocheza katika Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ wameteuliwa kwenye tuzo hiyo ambayo imebadilishwa mfumo wake baada ya ile ya Ballon d’Or ambayo Messi na Ronaldo wamekuwa wakipokezana kwa miaka minane iliyopita.

Kati ya hizo, Messi ameshinda miaka mitano na Ronaldo mara tatu hadi sasa. Mwaka huu, Ronaldo anapewa nafasi kubwa zaidi baada ya mafanikio yake akiwa ameshinda mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Real Madrid, Euro 2016 akiwa na Ureno.

Hata hivyo, Griezmann (25) ameng’ara na klabu yake, akimaliza nyuma ya Ronaldo kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya pamoja na Ulaya.

Klabu yake, Atletico Madrid na timu yake ya taifa yake Ufaransa, zilimshuhudia Ronaldo akiondoka na taji mwaka 2016, ambao Mfaransa huyo alikuwa kinara wa mabao Euro 2016.

Messi akiwa na miaka 29 amekuwa pia na msimu mzuri, kiwango bora akiiwezesha Barcelona kutwaa taji la La Liga na lile la Super, msimu wa 2015/2016, akifunga mabao 41.

Kwa upande wa wanawake, Mbrazili Marta ndiye anawania tuzo hiyo ambayo kura zake zitapigwa na manahodha wa timu za taifa na makocha, waandishi wa habari za michezo kutoka baadhi ya nchi kwa njia ya mtandao, mshindi atajulikana Januari 9.

Mbali ya Marta, wanasoka wa kile wengine ni, Melanie Behringer (Ujerumani/FC Bayern Munich) na Carli Lloyd (Marekani/Houston Dash).

Kiungo wa klabu ya Corinthians ya Brazil aliyefunga bao la ajabu kwenye mchezo wa Copa Libertadores dhidi ya klabu ya Chile, Cobresal atawania tuzo ya bao la juhudi binafsi akishindana na kinda wa miaka 17 raia wa Venezuela, Daniuska Rodrigue aliyefunga kwenye mashindano ya vijana ya soka wanawake chini ya miaka 17 na raia wa Malaysia, Mohd Faiz Subri, wa klabu ya FA Penang aliyefunga dhidi ya Pahang FC.

Wanaowania tuzo ya kocha bora wa mwaka ni Claudio Ranieri wa Leicester, kocha wa Ureno, Fernando Santos na Zinedine Zidane wa Real Madrid.