Guingamp yamnasa winga wa Guinea, Camara

Muktasari:

  • Hiyo ni baada ya winga huyo mwenye miaka 27, kuvunja mkataba wake na Derby County wiki iliyopita.Camara ambaye alijiunga na Derby akitokea klabu ya Ligue 1 ya Angers mwezi Januari 2016, amecheza mechi 26 na klabu hiyo ya England.

Klabu ya Guingamp inayoshiriki Ligi Kuu Ufaransa 'Ligue 1' imetangaza kumsajili nyota wa Guinea, Abdoul Camara.

Hiyo ni baada ya winga huyo mwenye miaka 27, kuvunja mkataba wake na Derby County wiki iliyopita.Camara ambaye alijiunga na Derby akitokea klabu ya Ligue 1 ya Angers mwezi Januari 2016, amecheza mechi 26 na klabu hiyo ya England. 

"Guingamp imevutiwa na nyota huyo baada ya kuridhika na kiwango cha Abdoul Razzagui Camara.

"Nyota huyo (27) atajiunga na En Avant kwa mkataba wa miaka miwili. "Razza" atavaa jezi namba 9 Cotes-d'Armor," ilisema taarifa ya klabu hiyo.

Camara, ambaye alichezea timu ya vijana ya Ufaransa, kabla ya kuchukua urai wa Guinea aliyoichezea mechi 12 na kufunga mabao manne.

Winga huyo amewahi kuzichezea klabu za Ufaransa za Rennes na Sochaux, pamoja na  Mallorca ya Hispania. Pia, amewahi kucheza  PAOK ya  Ugiriki.