Hili lishakuwa janga Barcelona kuumia kwa Suarez

Muktasari:

  • Suarez alipata majeraha wakati wa mchezo wa jana Jumatano wa Real Madrid na Barcelona kuwania taji la Super Cup ulioisha kwa vijana wa Zinedine Zidane kunyakua taji kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya kushinda mabao 2-0.

Hispania. Mshambuliaji wa Barcelona, Luis Suarez ameumia goti na anatakiwa kufanyiwa uchunguzi zaidi ili kubaini tatizo.

Suarez alipata majeraha wakati wa mchezo wa jana Jumatano wa Real Madrid na Barcelona kuwania taji la Super Cup ulioisha kwa vijana wa Zinedine Zidane kunyakua taji kwa jumla ya mabao 5-1 baada ya kushinda mabao 2-0.

Mchezaji huyo mwenye miaka 30 alionekana akiugulia maumivu kwenye goti la kushoto huku wachezaji wenzake wakimsaidia muda mfupi kabla ya madakri hawajaingia uwanjani.