Hofu ya kifo yampeleka McGregor kufuata mbinu kwa Mike Tyson

Marekani. Maandalizi ya pambano la ngumi baina ya Conor McGregor na Floyd Mayweather yamepamba moto ikiwa ni wiki chache baada ya mabondia  kuchimbana mkwara mzito kabla ya mchezo huo Agosti 26.

McGregor alitua kwa mkongwe Mike Tyson ili kupata mbinu mpya baada ya kuchimbwa mkwara kuwa atauliwa kwa makonde siku ya pambano.

Mchezo huo utakaopigwa jijini Las Vegas Marekani unasubiriwa kwa hamu, baada ya mabondi hao kutamba kila mmoja kuwa ataibuka mshindi, huku wakiendelea kurushiana maneno makali.