JKU yaifunza ujasiriamali Malindi

Muktasari:

Katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Fuoni, saa 8:00 mchana, mabaharia hao wa Malindi walionyesha bidii ili nao waokoke katika timu zinazoangaliwa kushuka daraja msimu huu.

Zanzibar. Maafande wa Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) wamezidi kuchanja mbuga kwa kushika nafasi ya pili katika Ligi ya Soka ya Zanzibar baada ya kuilaza  Malindi FC  kwa bao 1-0.

Katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Fuoni, saa 8:00 mchana, mabaharia hao wa Malindi walionyesha bidii ili nao waokoke katika timu zinazoangaliwa kushuka daraja msimu huu.

Mchezo huo ulianza kwa vuta ni kuvute kwa timu hizo ambako Malindi walionyesha soka la aina yake uwanjani  huku wakiwaacha mashabiki wao na matumaini ya ushindi kwenye mchezo huo.