James kutinga Anfield ikimaliza Top Four

Muktasari:

  • Nyota huyo wa kimataifa wa Colombia amekuwa hapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha Madrid chini ya Kocha, Zinedine Zidane na Desemba mwaka jana aliripotiwa akidai kwamba anaweza kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu baada ya kutua klabuni hapo katika dirisha kubwa la majira ya joto 2014 akitokea Monaco.

London, England .LIVERPOOL ina uhakika wa kumnasa kiungo mahiri wa Real Madrid, James Rodriguez kama ikifanikiwa kumaliza katika nafasi nne za juu baada ya staa huyo kudaiwa kuamua kuondoka Santiago Bernabeu mwishoni mwa msimu.

nyota huyo wa kimataifa wa Colombia amekuwa hapati nafasi katika kikosi cha kwanza cha Madrid chini ya Kocha, Zinedine Zidane na Desemba mwaka jana aliripotiwa akidai kwamba anaweza kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu baada ya kutua klabuni hapo katika dirisha kubwa la majira ya joto 2014 akitokea Monaco.

Inadaiwa kuwa Madrid pia imeipa ofa Chelsea kumchukua James wakati huu ikimnyemelea staa wa kimataifa wa Ubelgiji wa Chelsea, Eden Hazard lakini Liverpool ndio ipo katika nafasi nzuri zaidi ya kumchukua James baada ya kumfukuzia kwa muda mrefu sasa.