Jose Mourinho kuahirisha usajili wa wachezaji wawili hadi Januari mwakani

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho huenda akasitisha usajili wa msimu huu wa kiangazi na kusubiri wa mwezi Januari mwakani kutokana na mipango yake ya kuongeza wachezaji wawili kuonekana kukwama.

Dirisha la usajili simu huu, kocha huyo amewaingiza kikosini hapo Victor Lindelof, Romelu Lukaku na Nemanja Matic.

Usajili wa wachezaji hao umeghari Pauni 145 milioni. Awali, Mourinho alisema anataka kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji na winga lakini kila alipogusa kumtaka mchezaji mambo yamekuwa magumu.