Kilimanjaro Queens: Haikuwa rahisi kushinda

Muktasari:

  • Kilimanjaro Queens iliichapa Kenya maba 2-1 na kutwaa ubingwa wa mashindano hayo kwa mabao ya Mwanahamisi Omar “Gaucho’.

Dar es Salaam. Wachezaji wa timu ya Taifa ya wanawake “Kilimanjaro Queens’ wamesema haikuwa rahisi kushinda dhidi ya Kenya katika mchezo wa fainali ya Kombe la Chalenji uliofanyika nchini Uganda.

Kilimanjaro Queens iliichapa Kenya maba 2-1 na kutwaa ubingwa wa mashindano hayo kwa mabao ya Mwanahamisi Omar “Gaucho’.

Mfungaji wa mabao hayo, Mwanahamisi amesema wamefurahi kuchukua ubingwa huo na watahakikisha wanaendelea kujifua ili kuweza kutetea tena ubingwa wao mwakani.

mshambuliaji Asha Rashid ‘Mwalala’ amesema wadau mbalimbali waisapoti timu hiyo pamoja na ile ya Twiga Stars ili zizidi kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali yajayo.