Kinda wa U-20 Ghana aimezea mate Yanga

Kocha wa Yanga,Hans Pliujm

Muktasari:

  • Kinda huyo alikuwa akihaha muda wote kukutana na Kocha wa Yanga, Hans Pluijm kwa ajili ya kuzungumza naye huku akiwa na video zake katika simu kwa ajili ya kumshawishi.

Takoradi, Ghana. Kinda wa zamani wa timu ya Taifa ya Ghana (U-20), Awudu Zakari ameonyesha nia ya kutaka kuichezea klabu ya Yanga muda wowote atakapoitwa na miamba hiyo ya Tanzania.

Kinda huyo alikuwa akihaha muda wote kukutana na Kocha wa Yanga, Hans Pluijm kwa ajili ya kuzungumza naye huku akiwa na video zake katika simu kwa ajili ya kumshawishi.

Yanga ipo Ghana kwa ajili ya mchezo wake wa nne wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) uliochezwa dhidi ya wenyeji  wao, Medeama na kujikuta ikiburuzwa kwa mabao 3-1.

Zakari aliomba kukutanishwa na meneja wa mabingwa hao, Hafidh Saleh ambaye alieleza kumfahamu siku nyingi wakiwa wanawasiliana kama marafiki katika Facebook.

“Nasikia kuhusu Tanzania na nilikuwa nikiwasiliana mara kadhaa na Hafidh, kumbe ndiye meneja wao, natamani kuonana na kocha (Pluijm) nione kama ataniweka katika mipango yake.