Kipa wa Chelsea aitosa Real Madrid

Muktasari:

Raia huyo wa Ubelgiji, Courtois aliwahi kuichezea kwa mkopo Atletico Madrid na baadaye kujiunga na Chelsea na kufanikiwa kujiimarisha na kuwa kipa namba moja kwa msimu wa 2014/15.

London England. Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois amekiri kwamba ripoti zinazoenezwa kuhusu kujiunga na Real Madrid ni jambo lisilowezekana licha ya ukweli kwamba hiyo ni timu bora.
Raia huyo wa Ubelgiji, Courtois aliwahi kuichezea kwa mkopo Atletico Madrid na baadaye kujiunga na Chelsea na kufanikiwa kujiimarisha na kuwa kipa namba moja kwa msimu wa 2014/15.
Real Madrid inafikiria kumrudisha kipa wake aliyekwenda Manchester United mwaka 2015, David de Gea jambo ambalo linaonekana kugonga mwamba  na Keylor Navas anaonekana kupwaya katika msimu huu.
Hata hivyo, Courtois amezima matarajiao ya kwenda Madrid huku akiweka matumaini yake kuisaidia Chelsea katika mbio za kutwaa ubingwa wa Lig Kuu ya England msimu huu.
“Sitarajii kujiunga na Real Madrid,” alisema kipa huyo alipokuwa akizungumza na mtandao wa Cadena Ser.
“Nadhani Chelsea ndiyo sehemu sahihi kwangu hii ni klabu iliyoniona nikicheza Ubelgiji kwa miaka sita na ikaamua kunipa nafasi kikosini kwa knisajili.”
“Pia walinipa nafasi kucheza Atletico Madrid jambo ambalo limeniwezsha kufika hapa nilipo.”
“Ninajiona ni sehemu muhimu kwenye timu. Ninafurahia maisha ya soka Chelsea. Ninapenda zaidi kutembelea familia yangu inayoishi Real Madrid lakini ninafurahia maisha ya soka hapa London.”
Kikosi hicho cha Antonio Conte kimejiimarisha kileleni huku wakiwa na tofauti ya pointi 10 dhidi ya timu inayoifuatia ya Tottenham lakini wamebakiza michezo mingi mkononi.
“Tunafanya kazi vyema na Cote,” aliongeza Courtois.
“Ninadhani kazi kubwa iliyopo mbele yetu ni kutwaa ubingwa, siyo ligi ya nyumbani pekee hata mashindano ya barani Ulaya. Tunatamani sana kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.”