Friday, July 21, 2017

Kipa wa Madini aaga kimtindo

 

By Yohana Challe

Arusha. Kipa wa Madini Sc, Ramadhan  Chalamanda amesema hana mpango wa kuendelea kuichezea timu hiyo kwa msimu ujao.

Kipa Chalamanda aliyeiongoza Madini kucheza nusu fainali ya Kombe la FA msimu uliopita alisema alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo, lakini tangu wakati huo hadi sasa hana kiongozi yeyote wa Madini yamfuata ili kuzungumzia usajili wake.

“Mimi ni mchezaji mwenye umri mdogo, na lengo langu ni kufika mbali kwenye soka na sijaona tatizo wao kukaa kimya juu ya kunihitaji tena katika kikosi cha Madini,” alisema Chalamanda.

Aliongeza kuwa Madini itabaki  kwenye kumbukumbuku ya maisha yake kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata klabuni hapo japo kwa muda mfupi, lakini imemfanya  kujulikana.

Alishukuru uongozi wa Madini kwa kumwamini na kumfanya kuwa moja ya wachezaji watakao kumbukwa kutokana na uwezo wa wachezaji  walioonesha katika msimu wa ligi uliopita.

-->