Kiungo wa Yanga watafutia timu chipukizi

Muktasari:

Salvatory aliyeichezea Yanga kwa mafanikio  kwenye miaka ya 1990 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000 amewaongoza vijana wake hao jana kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Lipuli kwenye Uwanja wa Karume.

Dar es Salaam.  Kiungo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Salvatory Edward ' Doctor'  ameendelea kudumisha umoja na ushikamano kwa vijana wake aliwafundisha akiwa kocha wa vijana Yanga.

Salvatory aliyeichezea Yanga kwa mafanikio  kwenye miaka ya 1990 mpaka mwanzoni mwa miaka ya 2000 amewaongoza vijana wake hao jana kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Lipuli kwenye Uwanja wa Karume.

Kocha huyo alisema mbali ya kutengeneza umoja kwa wachezaji wake anatumia mechi hizo ili kuwauza vijana wake kwenye timu za Ligi Kuu Bara.

"Huwa nawapigia simu mara nyingi maana kila mchezaji  anasehemu anayofanyia mazoezi, najua uwezo wao maana wamepitia kwenye mikono yangu wengi wao.

"Hii inaendelea kutengeneza umoja na hata ushikamano wetu, lakini hiki ni kipindi cha usajili kuna ambao tayari wameonyesha uwezo  na mazungumzo yanaendelea. 

Katika hatua nyingine mara baada ya mchezo huo kumalizika bila kufungana kocha wa Lipuli, Suleiman Matola aligoma kuzungumzia vijana aliovutiwa nao katika kikosi cha Salvatory.

"Bado  mipango yangu haijakaa sawa, lingine hilo ni mapema mno kulizungumzia" alisema kocha huyo.

Lipuli itakaribishwa rasmi Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/2018  kwa kucheza mchezo wake wa kwanza dhidi ya bingwa mtetezi  Yanga, Agosti 27.