Kocha Mtibwa hofu tupu!

Kocha wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga .

Muktasari:

  • Mayanga aliyerejea Mtibwa kuchukua nafasi iliyoachwa na Mecky Maxime aliyejiunga na Kagera Sugar, alisema licha ya kufanya usajili wa wachezaji watatu bado kuna mahitaji ya wengine zaidi.

Dar es Salaam. Kocha wa Mtibwa Sugar, Salum Mayanga ameanza kuingiwa na hofu kuhusu ubora wa kikosi chake ukiwa ni mwezi mmoja kabla ya kuanza Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Mayanga aliyerejea Mtibwa kuchukua nafasi iliyoachwa na Mecky Maxime aliyejiunga na Kagera Sugar, alisema licha ya kufanya usajili wa wachezaji watatu bado kuna mahitaji ya wengine zaidi.

“Nimewasajili Rashid Mandawa, Haruna Chanongo na Cassian Ponera, lakini bado tuna pengo katika eneo la kiungo wa kati, kiungo wa pembeni na mshambuliaji.”

Nahodha wa timu hiyo, Vincent Barnabas alisema maandalizi ya timu kwa msimu ujao yanakwenda vizuri, wao kama wachezaji wamejipanga vyema ili kuziba nafasi zilizoachwa na wenzao walioondoka.