Friday, August 11, 2017

Kocha Omog kuwanoa kivingine Okwi, Bocco

 

By Thobias Sebastian @Mwananchi

Kocha wa Simba amepanga kuwanoa wachezaji wake, Mganda Emmanuel Okwi na John Bocco  ili kujindaa na na mechi ya pili ya kirafiki hapa nchini dhidi ya Singida United Jumapili Agosti 13, Uwanja wa Taifa.

Safu hiyo ya ushambuliaji ya Simba ambayo ilikuwa kiongozwa na Okwi pamoja na Bocco wameshindwa kuziona nyavu katika mechi hizo walizocheza nyavu.

Simba mpaka sasa wameshacheza michezo mitatu ya kirafiki kati ya Orlando Parates, ambao walifungwa 1-0, Bed Vets ambao walishinda 1-0, goli lilifungwa na Erasto Nyoni, yote ikiwa Afrika Kusini.

Pia, walicheza mechi nyingine hapa nchini dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda na Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0, lililofungwa na Mohammed Ibrahim 'MO'.

 

 

-->