Kocha Yanga nimefuata pointi tatu

Kocha Mkuu wa Yanga,Hans Van der Pluijim

Muktasari:

Pluijm anasema haoni kama mchezo huo kuna ugumu wowote  na kwamba anachohitajini alama tatu na kusonga mbele.

Mwanza. Kocha Mkuu wa Yanga,Hans Van der Pluijim amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Toto Africans ni kujichukulia pointi tatu na kuondoka.
Pluijm anasema haoni kama mchezo huo kuna ugumu wowote  na kwamba anachohitajini alama tatu na kusonga mbele.
“Tuko vizuri wachezaji wana ari,kwahiyo tunachotaka ni pointi tatu na kusonga mbele na lazima tushinde”anasema pluijim.
Pluijm aliongeza kuwa bado anaamini ubingwa wa msimu huu
watatutetea, kwani kupoteza mchezo mmoja siyo sababu ya kuwakwamisha kutwaa ubingwa tena.
“Nafasi bado tunayo ya kutetea ubingwa,wale Simba tutawapita na
nyinyi mtaona kumalizika kwa ligi,” alitamba Kocha huyo.